The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye…fuata Maelekezo -10

0

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

 

“Mama mimi sina uhusiano wowote na mume wako, wala sina mawazo hayo,” nilianza kujinasua mwenyewe ili kuweka hali salama…

“We koma!” alidakia mmoja wa wale wageni huku akinifuata.

 

JIACHIE MWENYEWE…

Nilikimbilia chumbani na kujifungia.

Sasa nikawa najiuliza, je, wale wageni walikuja kwa ajili ya kunishughulikia mimi au? Kwa nini wasiniulize maswali ambayo wangejua nani mkweli na mwongo?

Nilichukua simu na kumpigia baba Rehema haraka sana…

“Jamila vipi tena? Si kawaida yako!”

“Mama ameleta wageni nyumbani, wanataka kunipiga.”

“Nini?” aliuliza kwa mshtuko baba Rehema licha ya kwamba ilikuwa ndani ya simu lakini alionekana kama yupo sambamba na mimi chumbani.

Nilimsimulia kila kitu, baba Rehema akashangaa sana…

“Oke, niache nifanye kazi, nitajua nikija. Sasa hivi uko wapi sasa?”

“Nipo chumbani, nimejifungia mlango baba Rehema. Mimi najua nikitoka hao wenzake wanaweza kunijeruhi,” nilimwambia baba Rehema…

“Nakuja sasa hivi,” alisema na kukata simu.

Nilikaa kitandani nikilia. Sikujua kama mama Rehema angeweza kusema maneno kama yale mbele za watu na wao wakaamua kunichukulia hatua kama hii…

“Kwanza kama kweli ni binadamu mwenye kumuogopa Mungu  kwa nini asitumie lugha ya staa ya kusema huyu anaitwa Jamila ni msichana wangu wa kazi au ni dada wa kazi, yeye anasema huyu ni hausigeli wangu…mimi kwa kweli sijapenda,” nilijisemea moyoni.

Zilipita kama nusu saa, nikasikia sauti ya mama Rehema akiniita…

“Jamila.”

“Abee.”

“Unaitwa na baba Rehema.”

Nilisita kidogo, nilijua anataka nitoke ili anikabidhi kwa wenzake wanishughulikie.

Lakini nilipokumbuka kwamba, baba Rehema aliniambia atakuja sasa hivi, nikajua ni kweli, nikafungua mlango na kutoka.

Nilimkuta baba Rehema amekaa sebuleni na wale wanawake pia wapo…

“Kwani umelala?” aliniuliza baba Rehema…

“Hapana.”

“Sasa unafanya nini ndani chumbani muda huu?”

“Baba huyu mwanamke alitaka kunipiga,” nilianza kuwachongea…

“We binti wewe…mimi nilitaka kukupiga?” yule mwanamke alinijia juu…

“Ndiyo je!”

“Ilikuaje?” aliniuliza baba Rehema.

Nilisimulia kisa chote, mwanzo mpaka mwisho huku baba Rehema akionekana kukasirika kwa simulizi yangu. sikuongeza chumvi wala binzari na wala sikutaka kumsemea mtu kwa uongo…

“Mama Rehema,” baba Rehema aliita akiangalia chini kwa hasira…

“Abee…”

“Kwani haya ndiyo maisha unayoishi siku hizi hapa nyumbani?”

“Kivipi baba Rehema?”

“Kama wageni wako wanakuwa na ujasiri wa kutaka kumpiga mfanyakazi wa ndani mwangu, mimi mnaniweka katika nafasi gani ndani ya hii nyumba?” alihoji baba Rehema, hakuna aliyekuwa akisema neno, wote waliinamia chini wakati baba Rehema aliinua uso juu…

“Mimi sijapendezwa! Na kama mama Rehema haya ndiyo maisha nikiwa sipo, napingana na wewe kwa asilimia mia moja na natoa onyo kali nikisema kwamba, nyumba hii si sehemu ya eneo la unyanyasaji, binadamu wote ni sawa,” alipomaliza kusema hayo baba Rehema akasimana na kwenda chumbani kwake huku akisema nimuwekee juisi anatoka muda si mrefu.

Nikiwa kwenye kabati la vyombo nachukua glasi kwa ajili ya juisi, niliwasikia wale wanawake wakimuaga mama Rehema kwamba wanaondoka…

“Jamani mnisamehe kwa yote. Tena nawaomba sana sana niko chini ya miguu yenu, mnisamehe sana,” alisema mama Rehema kwa sauti ya chini sana huku wale wanawake wakiwa wameshasimama, yeye aliwasindikiza.

Niliweka juisi, baba Rehema akaja na kuinywa…

“Jamila,” aliniita akiwa ameshaanza kunywa…

“Abee…”

“Njoo mara moja.”

Nilikwenda sebuleni, akaniambia…

“Hebu kaa hapa.”

Nilikaa kwenye kochi dogo yeye akiwa kochi kubwa…

“Ondoa wasiwasi, amini upo kwenye nyumba salama. Hapa hakuna wa kukunyanyasa wala kukutoa zaidi ya mimi ninayekulipa mshahara, sawa?”

“Sawa…”

“Usiseme sawa, sema sawa baby,” baba Rehema alinielekeza…

“Sawa baby wangu, nakupenda sana,” nilisema nikamwongezea na zaidi kisha nikasimama na kwenda kumpa denda, akalikubali, tukajikuta tukiganda humo kwa muda.

Tuliganda tukashtuka baadaye, baba Rehema akasema…

“Umenikumbusha mbali, sasa unaweza kutoka humu ndani ukasingizia unakwenda saluni kuseti nywele?”

Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.  

Leave A Reply