The House of Favourite Newspapers

Huyu naye…Fuata Maelekezo-5

0

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
“Baba Rehema sitasema. Kwa nini niseme. Si nilikwambia nina miaka mingi, kwa hiyo siwezi kusema jambo la siri na kubwa kama hili.”
“Ngo ngo ngo,” geti kubwa la nje liligongwa, baba Rehema akakurupuka kutoka, nikamshika kwa nguvu na kumrudisha kitandani…
“Kwani we hujasikia geti limegongwa?” aliniuliza nikiwa nimemng’ang’ania.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
“Sasa mimi unaniachaje baba Rehema?” nilimuuliza bila kujali nini kitatokea endapo yule mama mpenda kula angeingia kwa njia nyingine na kutukuta kitandani, tena kwangu…
“Sikiliza Jamila…sikiliza kwanza…tutatafuta muda mwingine mwafaka tutamalizana…sawa?”
“Si sawa…basi ungetafuta kwanza huo muda mwingine tukamalizana kuliko hivi unavyotaka kunifanyia,” nilimwambia baba Rehema kwa sauti yenye kutetemeka maana tangu nilipoanza kazi pale kwake, sikuwahi kukatwa kiu. Ukijumlisha na ‘uchokozi’ wake, kwa kweli nilikuwa vibaya sana.
Nilikuwa nikihema kwa nguvu. Lakini sikujali. Geti lilizidi kugongwa lakini pia sikujali…
“Jamila si unasikia geti nje?” baba Rehema aliniambia…
“Agonge tu,” nilisema huku nikizidi kumvutia kwangu baba Rehema.
Nadhani baba Rehema alianza kuona ubaya wa kuchelewa kwenda kufungua geti, akatumia nguvu ya ziada ambapo alinizidi, akachomoka. Alivaa nguo zake huku akisema…
“Alaa! We unajua athari yake au unahisihisi tu hujawahi kupambana nayo? Tukikutwa humu chumbani, achilia mbali mimi hata wewe maisha yako yatakuwa hatarini.”
“Uliyataka mwenyewe lakini, mimi sikuwa na wazo hilo na nilikwambia,” nilimwambia huku nikijiweka sawa pale kitandani na yeye akawa ameshapotelea mlangoni.
Baada ya muda nilisikia sauti ya Rehema ikizungumza sebuleni huku akijibizana na baba yake…
“Haa! Kwa nini baba? Kwani mama hayupo?”
“Yupo ila ametoka kidogo.”
“Dada Jamila je?” aliuliza Rehema…
“Yupo chumbani kwake.”
Rehema alipitiliza hadi chumbani kwangu na kunisalimia. Baada ya hapo alitoka kwenda chumbani kwake. Mimi nikaitumia nafasi hiyo kwenda sebuleni ambako nilimkuta baba Rehema amekaa kwenye kochi kama mgeni wa nyumba hiyo…
“Vipi?” aliniuliza baada ya kuona nimesimama nikimwangalia tu.
“Poa, nani kaja?”
“Rehema…mbona unaniuliza wakati alikuja chumbani kwako?” aliniuliza baba Rehema.
Nilimfuata pale alipokaa, nikamkalia tena kwenye mapaja, akanisukuma…
“Tuko kwenye muda mbaya sana.”
“Kwako?” nilimuuliza.
“Wote tunahusika pia.”
“Nipeleke chumbani basi,” nilimwambia ili ikibidi anifanyie kama muda ule aliponibeba juujuu mpaka kwenda kunitupa kitandani, puu! Raha!

Jamila kwani huoni kwamba hali ya hewa si nzuri? Rehema amesharudi, sasa hivi atatoka…wewe unataka twende chumbani, kivipi?”
“Hawezi kutoka sasa hivi…mimi nina hali mbaya kuliko hiyo ya hewa unayoisema wewe,” nilimwambia huku nikimshika mkono.
Aliniangalia kwa kunikazia macho mara moja, kisha ghafla alisimama…
“Twende haraka sana,” alisema akiwa ameshaanza kutangulia mbele yangu.
Wakati tunapita kwenye mlango wa chumba cha Rehema, baba yake alifunga kwa funguo zilizokuwa zikining’inia kwa nje.
Tuliingia chumbani, mimi haraka sana nikapanda kitandani kwani nilishajua kwamba, baba Rehema alikuwa anacheza na muda na aliamua tu kuniridhisha mimi kwa vile nilikuwa nalialia sana…
“Hatukai lakini,” alisema akitupa nguo chini…
“Najua mbona,” nilimjibu huku na mimi nikiwa namalizana na nguo zangu.
Ile tunapuliza kipyenga cha kwanza tu kuashiria kuanza kwa mechi, Rehema akaita huku akipigapiga mlango…
“We dada Jamila…dada Jamila…”
“Mungu wangu, unamsikia huyo mtoto ameanza balaa,” alisema baba Rehema huku akiwa anapungukiwa na hali ya kujiamini…
“Dada Jamilaa…aaa!” aliita kwa nguvu akapiga mlango mba…mba mba!!!
“Nini wewe Rehema?” niliita na mimi ili kumuondoa kwenye kelele za kukata tamaa kwa kufungiwa…
“Nifungulie mlango bwana…kwa nini umefunga kwa nje?”
“Nakuja Rehema,” nilisema lakini tukiwa tayari uwanjani na baba yake.
Kwa haraka na wasiwasi, wala hatukufika dakika za kipindi cha kwanza mpira ukaenda mapumzikoni huku wote tukiwa na ushindi wa mojamoja!
“Tutafute muda mzuri, sawa?” alisema baba Rehema akivaa na kutoka haraka sana…
“Nani alikufungia Rehema?” aliuliza baba Rehema akijitoa kwenye kashfa ya kumfungia mwanaye chumbani…
“Si dada Jamila huyo…”

Kwa nini sasa?”
“Mimi sijui ni kwa nini!”
Rehema alitoka na kukaa sebuleni kisha akashika rimoti na kuanza kuminyaminya kutafuta vipindi vya katuni za watoto. Mara geti likagongwa tena. Hakukuwa na shaka kwamba safari hii ni mama Rehema…
“Jamila kafungue geti,” baba Rehema aliniambia na yeye akikaa sebuleni lakini kwenye kochi tofauti na alilokaa Rehema.
Ni kweli alikuwa mama Rehema…
“Shikamoo mama,” nilimsalimia…
“Kwenda huko…kwa siku unaamkia mara ngapi?” alinipa za uso. Nikakaa kimya, alipoingia nikafunga geti, tukaongozana kwenda ndani…
“Halafu we Jamila mbona unanuka mijasho namna hii?” mama Rehema aliniuliza huku akisimama kuniangalia kwa macho yenye mshangao…
“Sijaoga mama.”
“Halafu mama, leo dada Jamila alinifungia chumbani kwangu mpaka nikapiga kelele,” Rehema alinisemea kwa mama yake…
Je, nini kitaendelea? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.

Leave A Reply