The House of Favourite Newspapers

Huyu Ndo Dr Kidero Anayedaiwa Kumiliki Mali za Mabilioni Kimagumashi

Image result for Dr. Evans Kidero

TUME ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC) nchini Kenya imechapisha ripoti ya mali mbalimbali zinazomilikiwa na aliyekuwa Gavana wa Jiji la Nairobi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Sukari ya Mumias, Dr Evans Kidero, ambazo ripoti hiyo imesema hakuzipata kihalali.

 

Kidero amefunguliwa mashitaka katika mahakama ya Nairobi akituhumiwa kwa ubadhirifu na makosa mawili ya kupotea kwa fedha za umma, makosa ambayo yamejumuisha bilioni 9 za Kenya wakati akiwa katika nyadhifa sehemu hizo mbili.

Full list! Dr. Evans Kidero multi million properties that have left Kenyans in total distress

 

Dr Kidero amesema utajiri huo aliupata kihalali na kwamba tume hiyo inatafuta njia za kumuumiza na kumdhalilisha.

Orodha ya mali hizo ambazo ni pamoja na majengo na ardhi ni:

–          Ghorofa la Yala Towers jijini Nairobi (lenye thamani ya sh. bilioni 1.2 za Kenya)

–          Ghorofa la Muthaiga Heights (bilioni 1)

–          Nyumba 50 za kupangisha Barabara ya Riara Nairobi (bilioni 1)

–          Nyumba za Gem zilizoko State House Crescent (bilioni 1)

–          Nyumba za Gem zilizoko Rose Avenue (milioni 700)

–          Nyumba za Gem zilizoko Gigiri (milioni 100)

–          Nyumba 4 eneo la Nyari,  Nairobi (milioni 800)

–          Mali zilizoko Ndege Road eneo la Karen (milioni 600)

–          Nyumba zilizoko Riverside (milioni 500)

–          Nyumba yake ya Muthaiga (milioni 300)

–          Nyumba eneo la  Rosslyne karibu na Runda (milioni 100)

–          Nyumba Riverside Drive (milioni 90)

–          Massionates in Lake View Estate Kisumu (milioni 200)

–          Hekta 50 za ardhi Kisumu (milioni 100)

Kidero anasemekana pia ana mashamba huko Kisumu na Homabay na magari ya kifahari 11.

Comments are closed.