The House of Favourite Newspapers

Ibada Kumuaga Dada wa Shigongo Yafanyika Bupandwamhela (Pichaz)

Jeneza lenye mwili wa Vaileth baada ya kuwasili katika ukumbi wa ibada nyumbani Bupandwamhela.

IBADA ya kuuaga mwili wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, imefanyika leo Ijumaa, Juni 21, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza.

 

 

Mwili wa Vaileth ambao uliwasili nyumbani kwao jana Alhamisi kutokea nyumbani kwake, Nyamhongolo jijini Mwanza, utazikwa leo kijijini hapo katika eneo la makaburi ya familia.

 

Dada wa marehemu na ndugu wengine wakiwa katika ibada.

 

Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, vyama, taasisi na mashirika mbalimbali wamefika nyumbani hapo kwa ajili ya kuungana na waombolezaji kuuaga na kuusindikiza mwili wa mpendwa wao huyo katika nyumba yake ya milele.

 

Waombolezaji wakiwa katika ibada.

 

Ibada fupi ikifanyika ndani kabla ya mwili kupelekwa ukumbini kwa ibada kubwa ya kuaga.

 

…Ibada fupi ikiendelea.

 

Shigongo akiwa na watoto wa marehemu, Deus na dada yake wakati wa ibada.

 

Mwili ukipelekwa ukumbini kwa ajili ya ibada ya kuaga.

 

 

Ndugu wa marehemu wakiwa wenye huzuni.

 

Taswira ya huzuni iliyotawala ibada.

 

….Ni masikitiko matupu!

 

Mhariri mwandamizi wa Global Publishers, Elvan Stambuli (kulia),  akiwa katika ibada.

 

PICHA NA DENIS MTIMA NA IDD MUMBA | GPL

Comments are closed.