The House of Favourite Newspapers

IBADA YA KUBARIKI MAKABURI YA WAZAZI WA SHIGONGO YAFANYIKA MWANZA

LEO, leo Jumatatu, Desemba 24, 2018, familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, imefanya ibada maalum ya kuwaombea marehemu wazazi wao ambao ni Baba yao Mzee James Bukumbi na mama yao, Bi. Asteria Kapela pamoja na marehemu wengine wa familia hiyo ambao walikwisha fariki dunia.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yakobo Mkuu, Parokia ya Mwangika, Padri Faraja Hilali, baada ya maombi na misa, padri huyo alibariki makaburi ya Baba wa Shigongo, Mzee James Bukumbi na la mkewe, Bi Asteria Kapela yaliyopo nyumbani kwao, Kijiji cha Bupandwamhela, Sengerema Mwanza.

Padri Faraja pia amebariki makaburi ya ndugu wa familia hiyo yaliyopo hapo nyumbani na mengine yaliyopo katika kijiji jilani cha Kafunzo.

deGE

Comments are closed.