The House of Favourite Newspapers

Ibenge Mguu Mmoja Simba

0

SI mara kwanza jina la Jean-Florent Ibengé kutajwa kwenye soka la Tanzania, safari hii anahusishwa kuinoa Simba baada ya kuondoka kwa Kocha Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji.

 

Ibenge ambaye ni Kocha wa Timu ya Taifa ya DR Congo na Klabu ya AS Vita ya nchini humo, awali alikuwa akihusishwa na Yanga kabla ya ujio wa Cedric Kaze anayeinoa timu hiyo kwa sasa.

 

Hivi karibuni, Sven aliondoka ghafl a kwenye kikosi cha Simba kabla ya uongozi wa timu hiyo kutoa tamko la kuachana naye ikiwa ni muda mchache baada ya kuifi kisha timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinasema kwamba, Ibenge ameibua mvutano ndani ya klabu hiyo kutokana na baadhi ya viongozi kumhitaji, huku wengine wakimtaka Kocha Rene Wailer aliyewahi kuinoa Al Ahly.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba, kimesema kuwa viongozi wengi wa timu hiyo mawazo yapo kwa Ibenge hiyo ni kutokana na historia yake nzuri kwenye mashindano ya kimataifa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Simba wametinga hatua ya makundi na wanataka kufanya kweli awamu hii.“

 

Kocha ambaye viongozi wanamhitaji kwa sasa ni Ibenge, kama ambavyo unajua mafanikio ya kocha huyo kwenye mashindano ya kimataifa.“Hivyo viongozi wanamtaka ili aje atusaidie kwenye Ligi ya Mabingwa katika hatua hii ya makundi kwa sababu lengo letu ni kufanya vizuri zaidi msimu huu,” kilisema chanzo.Ibenge ambaye ni mzaliwa wa Kinshasa DR Congo, kwa sasa umri wake ni miaka 59.

 

ATUA BONGO, MO ARAHISISHIWA KAZI

 

Dili la Ibenge kujiunga na Simba huenda likawa mtelezo kwa uongozi wa klabu hiyo kutokana na kocha huyo jana Jumamosi mchana kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa na kikosi cha DR Congo.Ibenge amekuja na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa kirafi ki dhidi ya Taifa Stars utakaopigwa Januari 12, mwaka huu kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

 

Ujio huo wa Ibenge utawapa nafasi Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ kuweza kumbana na kumalizana naye hapahapa bila ya kusubiri kumfuata kwao DR Congo.

SVEN AIBUKIA MOROCCOWAKATI

anaondoka Simba, Sven alitaja sababu kubwa ya kuachana na timu hiyo ni kuhitaji kuwa karibu na familia yake, huku akikataa kabisa kuhusu kupata dili lingine.Jana mchana, zilitoka taarifa kwa, Mbelgiji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa FAR Rabat inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

 

Sven anaenda kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Abderrahim Talib ambaye amefutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo.FAR Rabat katika ligi kuu ya nchini humo, wanashika nafasi ya 11 kati ya timu 16 ambapo katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa, wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, huku wakitoa sare mbili na kupoteza mbili. Wamekusanya pointi tano.WAANDISHI: Ibrahim Mussa, Issa Liponda na Marco Mzumbe

Leave A Reply