Ibraah Amkana Mrembo Aliyemchora Tattoo

MIONGONI mwa stori zinazotrendi kwa sasa ni ile inayomhusu msanii Ibraah kutoka Lebo ya Konde Music Worldwide ambaye amekana kuwa kwenye penzi na msanii wa filamu na video vixen Nanah aliyechora tattoo ya jina lake shingoni.

 

Ibraah amesema kuchorwa tattoo na mrembo huyo haihusiani kwamba ndio wapo kwenye mahusiano bali kilichokuwepo kwao ni upendo na urafiki.

 

Nanah sio mtu wangu ni rafiki yangu na ana mahusiano yake, kuhusu tattoo kila mtu anaamua kuchora, nilivyomuona nilimuuliza akasema amependa tu kuchora jina la Ibraah kwa sababu mimi ni mtu wake wa karibu na nina umuhimu kwake, mbona kuna watu wengi wamenichora ila wanamsema Nanah tu,” amesema Ibraah.

 

Pia ameendelea kusema urafiki wao kwa sasa una muda wa miezi 6 na kinachoendelea kati yao ni upendo tu.Tecno


Toa comment