The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrity: Ice Boy Azungumzia Single Yake Mpya ‘Binadamu’ Adai Haihusiani Na Young Killa ILA… – ( Video)

Camera za Global TV Online zilikutana na msanii wa Hip Hop Ice Boy na kupiga nae stori mbili tatu. Kwenye interview, msanii huyo alituambia vitu vingi ikiwemo safari yake alivyoanza muziki pamoja na sababu za kutunga kwa single yake ya sasa ‘Binadamu’.

Ice Boy ameiambia Global TV Online sababu zilizomsukuma mpaka kuandika single yake mpya ‘Binadamu’, kwa maneno yake binafsi; “hii ngoma inagusa watu wengi, wale wote wanao-struggle kila siku…

Akizungumza  na Global TV Online, Ice Boy aliendelea kuiongelea ngoma hiyo akisema:

‘Binadamu’ imebase sana kwenye maisha yangu ya ukweli, inagusa karibia asilimia sabini ya maisha yangu mimi, hustle zangu, mishemishe, jinsi watu walivyonizingua na kunikunjia nisifike sehemu. Hii ngoma inagusa pia maisha ya watafutaji wengi wanao-struggle na maisha kila siku… ” – Ice Boy.

Mbali na hayo kumekuwa na tetesi kuwa ngoma hii kwa upande mmoja imemlenga msanii wa Hip Hop Young Killa, Ice Boy alilizungumzia hilo kwa kusema:

Sitaki kumuongelea mchizi, nimesema hii ngoma inahusu maisha yangu so kama aliwahi kunikunjia basi itakuwa inamhusu… ” – Ice Boy.

Kuicheki interview nzima ya Ice Boy na Global TV Online bonyeza play hapa chini.

Itazame tena video ya Ice Boy ‘Binadamu’ Feat. Nandy hapa chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Interview/ Video: Becka Issa.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 

Comments are closed.