Idadi ya Watu Duniani Sasa Bilioni 7.7, Tanzania Mil 60

KWA mujibu wa takwimu zilizotolewa juzi na Shirika la Umoja wa Mataifa katika kitengo cha takwimu za ongezeko la watu ulimwenguni, zimeonyesha kuwa duniani kuna watu bilioni 7,713,468,000 huku Nigeria ikiwa nchi pekee yenye idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake.

 

Takwimu hizo zimeonyesha kuwa ongezeko la watu duniani litaongezeka hadi Bilioni 8.9 ifikapo mwaka 2030, na bilioni 9.7 ifikapo mwaka 2050, na hadi bilioni 10.9 ifikapo mwaka 2100.

 

Nigeria imeripotiwa kuwa na watu milioni 200,964,000 hadi kufikia katikati mwa mwaka 2019, katika idadi hiyo wanawake wamekuwa milioni 99,132,000 huku wanaume wakifikia milioni 101,832,000.

 

Hata hivyo, takwimu hizo zinaonyesha  duniani kuna wanaume milioni 3,889,035,000 na wanawake milioni 3,824,434,000, huku Tanzania ikifikisha watu 60,855,477, hii ni kwa mujibu wa takwimu hizo mpya.

 


Loading...

Toa comment