The House of Favourite Newspapers

Idris Ataja Sababu Kumficha Mpenzi Wake

0

MWIGIZAJI wa kimataifa wa Tanzania ambaye ni Mshindi wa Shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan ametaja sababu inayomfanya kumficha mpenzi wake kwa kutomposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa ni kutaka kuwa huru na maisha yake binafsi.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Idris ambaye miezi kadhaa iliyopita aliwatoa Wabongo kimasomaso baada ya kushiriki kwenye filamu zinazoandaliwa na mtandao wa filamu duniani wa Netflix anasema tangu ameachana na Wema Sepetu, aliamua kufanya siri uhusiano wake wa kimapenzi ili maisha mengine yaendelee.

“Nilishaweka sana uhusiano wangu hadharani, sasa ni wakati wa kufanya siri, nimeamua kufanya hivi kwa sababu mitandaoni kuna mambo mengi, lakini pia nataka mashabiki wangu wanifuatilie mimi zaidi kwenye kazi zangu na sio maisha yangu ya kimapenzi.

“Hali hii nimeipenda kwa sababau hivi sasa hata nikiwa na mwanamke watu hawatajua na kama tukishindwana basi tunaachana kimyakimya na maisha mengine yaendelee,” anasema Idris.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply