The House of Favourite Newspapers

Idris Kuja na Sapraizi Baada ya Mfungo

0

STORI: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI| ShowBiz

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Idris Sultan amefunguka kuwa baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Mfungo wa Ramadhani amejipanga kutoka na sapraizi kwa mashabiki wake wa mitindo ya bidhaa yenye nembo ya Sultan ambayo itampeleka kwenye levo za kimataifa.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Idris aliongeza kuwa bidhaa hiyo ambayo hayupo tayari kuiweka wazi moja kwa moja, mbali na kumpeleka kimataifa lakini itamtofautisha na wanamitindo wengi wanaofanya kazi zao kwa mazoea.

“Kwa sasa watu wapo katika mwezi wa mfungo, kwa hiyo niwaache waendelee na mfungo lakini tukifungua tu watakutana na sapraizi ya hatari kutoka kwangu itakayomfurahisha kila mtu, mashabiki wangu wawe tayari kwa kitu kizuri,” alisema Idris.

Leave A Reply