The House of Favourite Newspapers

IDRIS SULTAN APATA DILI NONO SAUZ

Idris Sultan

MSHINDI wa Big Brother Afrika 2014 na mchekeshaji, Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la  Komedi lililoandaliwa na Comedy Central, moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini (Sauz).

 

Mwaliko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo  wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu  ya wapenzi wa comedy hapa nchini.

 

Idris amesema mwaliko huo  ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

 

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour, Idris alisema lilikuwa na lengo kuu la kuburudisha na kuelimisha watu katika maswala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji. “Tarehe 1 Desemba, Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar ambapo watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket. 

Sex Tour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini  Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa  ya muziki” anasema likibeba ujumbe “Kutokupima hakubadili matokeo” tamasha hilo lilihudhuriwa na  wachekeshaji mbali mbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu,  Dogo Pepe, Coy Mzungu, Blackpass, Kitenge, Nalimi, Optalema Deo, Max, Young Unstopable ,D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass.

“Changamoto za maambukizi mapya kwa vijana wa umri 15-24 bado ni kubwa, hivyo Sex Tour ilikua inalenga zaidi kushauri vijana kujali afya zao, kutokuwa na hofu ya  kupima afya zao lakini pia kubadili fikra potovu za kuwa nyanyapaa wenye maambukizi,” anasema Idris  Tamasha la Sex Tour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania.

HABARI: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.