The House of Favourite Newspapers

IDRISS ADAIWA KUJISOGEZA KWA MOBETO

Idris Sultan

MADAI yanayosambaa kama moto wa kifuu ni juu ya mchekeshaji maarufu  Bongo, Idris Sultan  kudaiwa kujiweka kwa mwanamitindo, Hamisa Mobeto.  

 

Shushushu wetu aliitonya Za Motomoto kuwa, Idris kwa sasa ameamua kujipooza kwa Mobeto. “Wamekuwa wakiongozana kila kona kama kumbikumbi, ndiyo kwanza mapenzi yao yanachipukia,” alisema shushushu huyo.

 

Za Motomoto ilimtafuta Idris kujua ukweli wa hili ambapo alipopatikana aligeuka mbogo kwa kusema siyo kila mwanamke anayeongozana naye ni mpenzi wake.

“Hebu acheni mambo yenu ya ajabu bwana kwa hiyo kila msichana nitakayeongozana naye basi ni mpenzi wangu? Halafu mmesahau kwamba mimi na Hamisa ni washkaji kitambo tu? Sasa kwa nini leo muanze kusema natoka naye? Muda mwingine watu wakikosa kazi ya kufanya huwa wanatunga tu vitu vyao,” alisema Idris.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.