IFAHAMU PRESHA YA KUSHUKA (HYPOTENSION)
PRESHA ya kupanda ndio maarufu duniani lakini ipo presha ya kushuka ambayo nayo ni hatari. Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka (90/60 mm Hg) ambayo huonekana kutokuwa na sababu iliyoifanya itokee. Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyingine huwa chini. Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko. Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao.
Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huwa ni dalili ya presha ya kushuka pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa.
Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana kama postural hypotension au orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension.
Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasiliano unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu. Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari, kama vile mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uliopo.
Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile.
Ikiwa jambo hili halikufanyika au limefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaanguka ghafla. Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka.
itaendelea wiki ijayo.
Comments are closed.