The House of Favourite Newspapers

Ifahamu Treni ya Kasi Zaidi Afrika

Morocco imezindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika – itakayopunguza nusu ya muda unaotumika kusafiri katika miji ya biashara na viwanda ya Casablanca na Tangier.

 Mfalme wa Morocco, Mohammed VI na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,  waliipanda treni hiyo katika safari ya uzinduzi kutoka Tangier hadi katika mji mkuu, Rabat.

Rais wa Ufaransa Eammanuel Macron (kushoto) amealikwa katika uzinduzi wa treni ya kasi, Morocco.

Takwimu kuhusu treni hiyo:

  • Treni imepangiwa kwenda kwa kasi ya kilomita 320 kwa saa
  • Itakapunguza kwa zaidi ya nusu muda unaotumika kusafiri km 200 kutoka mji wa Casablanca hadi Tangier kuwa safari ya saa mbili.
  • Inakwenda kwa kasi ya mara mbili zaidi kuliko treni ya mwendo kasi ya Afrika Kusini inayouunganisha uwanja wa kimataifa wa ndege wa Johannesburg na mji wa biashara wa Sandton.
  • Inagharimu dirham bil. 22.9 ($2.4bn; £1.8bn), kwa mujibu wa shirika la habari la kitaifa MAP.
  • Ilichukua miaka saba kuijenga reli ya treni hiyo.

Afrika inatazamia kuimarisha miundo mbinu ya usafiri katika biashara, uwiano na utangamano wa kieneo. Mataifa ya Afrika yanakumbatia mfumo wa reli ya mwendo kasi katika kukuza uchumi na kuimarisha kasi za kusafirisha bidhaa baina ya mataifa kibiashara.

Comments are closed.