The House of Favourite Newspapers

Sirro: Anayetaka Siasa Afanye, Anayetaka Shari… – Video

0

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewaonya wanasiasa walioanza kuonYesha shari kupitia matamshi yao kuelekea uchaguzi mkuu, Oktoba 2020 na kuwataka kutolilaumu jeshi lake litakapochukua hatua dhidi yao.

Amesema, “Nimeona viongozi wa siasa wanazungumza mambo makali sana. Ninawaheshimu viongozi wote wa siasa katika ngazi zote lakini lazima sheria na kanuni zilizopo ziheshimiwe.”

Ameongeza, “Ukiangalia baadhi ya viongozi wanavyozungumza unaona kuna ushari wanaouonyesha wanaupeleka kwa washabiki wao wawe na ushari huo. Wao wanachozungumzia si uchaguzi wa amani na utulivu, sera yao ni ushari.

Aidha, amesisitiza, “Niwaombe sana, anayetaka kufanya siasa afanye siasa, anayetaka kufanya ushari aache mapema. Unamkuta kiongozi mkubwa anazungumza maneno ya ukali sana, anasahau amepata nafasi ya kuzungumza kutokana na amani iliyopo. Kama siyo amani angekuwa chini ya uvungu wa kitanda chake.”

 

Leave A Reply