The House of Favourite Newspapers

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO KTK JESHI LA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemteua aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Ahmed Msangi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar

 

Nafasi aliyokuwa DCP Msangi ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi inachukuliwa na Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime.

 

Aidha, aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Maulid Mabakila amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Jijini Dar

Comments are closed.