Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, ametoa wito kwa Watanzania na wasio Watanzania kuacha kufanya vitendo vya uhalifu na kukimbilia kujificha nchi nyingine kwani kwa sasa kuna mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba mtu yeyote atakayefanya uhalifu anakamatwa popote pale atakapokimbilia.
IGP Sirro ametoa wito huo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliowakutanisha Wakuu wa Jeshi la Polisi wa nchi zote zinazounda Umoja wa Kusini mwa Afrika (SADC).
Comments are closed.