The House of Favourite Newspapers

Ihefu FC Kuivaa Yanga Kwa Tahadhari

0

KOCHA wa Ihefu ya mkoani Mbeya, Zuberi Katwila amesema kuwa tayari kikosi chake kipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na Yanga SC huku wakiwa na tahadhari kubwa dhidi ya wapinzani wao hao.

 

Ihefu inatarajia kukutana na Yanga kesho kwenye Dimba la Mkapa kwa ajili ya kutafuta pointi tatu zitakazowasaidia kujiweka sehemu nzuri ya kuepuka kushuka daraja.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Katwila alisema kuwa, mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa upande wao ili kujihakikishia usalama wa kubaki ligi kuu msimu ujao.

 

“Tumekuja kwa tahadhari ya hali ya juu kwa sababu tunaenda kushinda na timu kubwa na yenye uwezo mkubwa pia kwa hiyo tupo sana katika mchezo huu na tumejipanga vizuri.

 

Wachezaji wote wapo salama kabisa na wote kwa pamoja tumekuja kutafuta pointi tatu zitakazotusaidia kuepuka na hatari ya kushuka daraja,” alisema Katwila.Ihefu hadi sasa imekusanya pointi 35 katika michezo 32 iliyocheza ya ligi Kuu Bara na kupata ushindi katika michezo tisa, wamepoteza 15 na kutoa sare nane.

Stori: Hawa Aboubakhari,Dar es Salaam

Leave A Reply