The House of Favourite Newspapers

Ihefu Watangaza Kumhofia Bocco Simba

0

NAHODHA wa timu ya Ihefu, Joseph Kinyozi amefunguka kuwa kitu pekee kinachowapa hofu kwenye mchezo wao dhidi ya Simba utakaochezwa leo Jumatano Uwanja wa Mkapa ni uwepo wa John Bocco na Luis Miquissone uwanjani.

 

Kinyozi amesema Bocco na Luis ni wachezaji hatari zaidi kwenye ligi ya Bongo kiasi ambacho kinawapa hofu na kuwaza ni namna gani wataweza kuwazuia ili wasilete madhara kwenye lango lao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kinyozi alisema licha ya kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea kwenye mchezo huo lakini bado hawana imani kila wanapowaza uwepo wa Bocco na Luis kwenye kikosi cha Simba, kwa kuwa nyota hao wana uwezo wa kufanya jambo lolote na wakati wowote wakiwa uwanjani.“

 

Tumefanya maandalizi ya kutosha kuelekea kwenye mchezo wetu na Simba hiyo kesho (leo), lakini bila kuficha Bocco na Luis ni wachezaji ambao wanatupa hofu sana, wale wakiwa uwanjani muda wowote wanaleta hatari, kucheza na watu kama hao siyo jambo rahisi. Inahitaji umakini na nidhamu ya juu sana kwa sababu hata sisi tunajifunza mengi kupitia kwao,” alisema Kinyozi.

Issa Liponda,Dar es Salaam

Leave A Reply