The House of Favourite Newspapers

IJUE MIJI 3 YA AJABU CHINI YA BAHARI UNAYOPASWA KUITEMBELEA

Lion City – Qiandao Lake, China
Mji huo ulifurikishwa maji kwa makusudi mwaka 1959 ili kujenga ziwa na kituo cha umeme kinachotumia nguvu za maji.  Lion City (uliochukua jina la Lion Mountains) ulikuwa kituo cha kisiasa na kiuchumi mashariki mwa China.

Antirhodos – Alexandria, Misri
Kisiwa hiki cha chini ya maji kinaaminia kilizama kutokana na matetemeko ya ardhi katika karne ya nne.  Kiligunduliwa karibu na bandari ya  Alexandria mwaka 1996.  Mtu unabidi ufike hapo ili uamini.

Dwarka – India
Uko chini ya maji  (futi 70) ambazo ni mita 21 karibu na kisiwa kinachokaliwa na watu cha  Bet Dwarka.  Mji huo wa zamani wa Dwarka ni hazina ya kweli ya zamani unayopaswa kuitembelea.  Unakisiwa kuwa ulijengwa kati ya miaka  9,000 na  12,000 iliyopita.

Comments are closed.