The House of Favourite Newspapers

Ijumaa Figa Bomba Girl 2017: Kalio la Kichina Latikisa

0
Modo mwenye figa bomba, Jane Ramoy ‘Sanchi’.

SHINDANO bab’ kubwa ambalo linatikisa kila kona la kumtafuta staa wa kike mwenye figa bomba linazidi kupamba moto ambapo wadada watatu walioingia fainali, Wema (Namba yake  18) , Sanchi  (Namba yake  25) na Sasha (Namba yake  12)  wanaendelea kutifuana.

Huku kila mmoja kwa wakati wake akijinadi kuwa yeye ndiye mwenye shepu bomba kuliko wenzake, huko mtandaoni kwenye ukurasa wetu wa Facebook wenye jina la Gazeti la Ijumaa na kurasa za kijamii za Global Publishers ambako kila siku tunatupia mapicha yao, mjadala mkubwa umekuwa kwamba, eti figa zao zina uhusiano mkubwa na ‘Mchina’.

Mwanamitindo, Sasha Kassim.

“Duu! Hawa mabinti wana shepu bomba kinoma, kama kweli ndivyo walivyo basi Mungu kawapendelea lakini nahisi watakuwa wanatumia dawa za Kichina kama siyo kujaladia,” alisema mmoja wa wafuatiliaji wa shindano hilo mtandaoni aliyejitambulisha kwa jina la More P.

Mbali na huyo, wengi wamekuwa wakikomenti na kuhoji uhalisia wa makalio ya mastaa hao huku hoja kubwa ikiwa ni kwamba, mbona baadhi ya picha makalio yao si makubwa kivile?

 

Hata hivyo, mratibu wa shindano hili, Andrew Carlos ameeleza kuwa, washiriki wote walioingia fainali shepu zao ni orijino na ili kuamini hilo tembelea ukurasa wetu wa Facebook na kurasa zote za kijamii za Global Publishers pamoja na Global TV Online ambapo utaona mapicha yao wakiwa na bikini na mizigo yao ikionekana wazi.

 

Staa wa Bongo, Wema Sepetu.

Wewe msomaji unadhani nani ana figa bomba kuliko wenzake? Ili kushiriki katika kumpata mshindi, chukua simu yako, nenda sehemu ya kuandikia SMS kisha andika neno SHEPU acha nafasi, andika namba ya mshiriki unayetaka awe mshindi kisha tuma kwenda namba 15542. Hii ni kwa wateja wa Vodacom pekee.


Leave A Reply