Ijumaa Sexiest Girl 2019… Bye Queen Elizabeth!

ZOEZI la kupiga kura linazidi kushika kasi ambapo baada ya msanii wa Bongo Fleva, Rosa Ree (17) kutolewa, wiki hii hali imekuwa mbaya kwa Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth (19) ambaye ameambiwa bye na wapiga kura.

 

Warembo 20 waliingia kwenye kinyang’anyiro cha kupigiwa kura na wasomaji katika shindano hili la kumtafuta Mrembo Mwenye Mvuto wa Gazeti la Ijumaa (Ijumaa Sexiest Girl 2019).

 

Mratibu wa shindano hili ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul amesema baada ya Rosa Ree, wiki hii upepo ulikuwa mbaya kwa Queen Elizabeth kufuatia kupigiwa kura nyingi za kutoka.

 

“Zoezi la kupiga kura sasa limeshika kasi ya ajabu, baada ya Rosa Ree, sasa ni Queen Elizabeth.

“Washiriki waliobaki ni Nandy (1), Lulu Diva (2), Lulu (Elizabeth Michael) (3), Kidoa (4), Sanchi (5), Official Lyyn (6), Tunda (7), DJ Sinyorita (8), Amber Lulu (9) na Wolper (10).

 

“Wengine ni V-Money (11), Diana Kimari (12), Poshy Queen (13), Mimi Mars (14), Kim Nana (15), Official Nai (16), Malkia Karen (18) na Sylivia Sebastian (20).

 

“Unachotakiwa kufanya ni kupiga kura ya nani atoke kwa kuandika jina au namba yake ya ushiriki kisha unatuma kwenda WhatsApp namba; 0713 750 910,” alisema Sifael na kukaribisha wadhamini mbalimbali kwenye kinyang’anyiro hicho.

 

IJUMAA SHOWBIZ

Toa comment