The House of Favourite Newspapers

Ijumaa Sexiest Girl 2019… Kipyenga Kimepulizwa

BAADA ya wiki iliyopita kuanika 10 bora nyingine ya shindano bab’kubwa la kumtafuta Mrembo wa Gazeti la Ijumaa (Ijumaa Sexiest Girl 2019), habari ikufikie kuwa hii sasa ndiyo Top 20 ya washiriki wote.

 

Mratibu wa shindano hili ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul amewapongeza wote walioshiriki kuchagua 10 bora ya kwanza na hii ya pili.

“Nawashukuru wote walioshiriki kutuma majina ya washiriki, hii inaonesha shindano hili safari hii litakuwa la kitofauti.

“Sasa washiriki wetu wapo 20 ambao ni Nandy (1), Lulu Diva (2), Lulu (Elizabeth Michael) (3), Kidoa (4), Sanchi (5), Official Lyyn (6), Tunda (7), DJ Sinyorita (8), Amber Lulu (9) na Wolper (10).

 

“Wengine ni V-Money (11), Diana Kimari (12), Poshy Queen (13), Mimi Mars (14), Kim Nana (15), Official Nai (16), Rosa Ree (17), Malkia Karen (18), Queen Elizabeth (19) na Sylivia Sebastian (20).

 

“Baada ya kupata listi hii, kifuatacho ni utaratibu wa kupiga kura za nani atoke na nani abaki ambao utaanza rasmi wiki ijayo,” alisema Sifael akiwakaribisha wadhamini mbalimbali wa kinyang’anyiro hicho.

SHOWBIZ, Dar es Salaam

Comments are closed.