The House of Favourite Newspapers

IJUMAA SEXIEST GIRL 2019… ROSA REE OUT!

0

KURA zimeanza kupigwa kwa spidi ya ajabu ambapo wiki hii msanii wa Bongo Fleva, Rosa Ree (17), ameoneshwa mlango wa kutokea (out).

 

Wiki iliyopita ilianikwa listi ya warembo 20 watakaokuwa wakipigiwa kura na wasomaji katika shindano hili baab’kubwa la kumtafuta Mrembo wa Gazeti la Ijumaa (Ijumaa Sexiest Girl 2019).

 

Mratibu wa shindano hili ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul amesema baada ya kuanika listi hiyo, zoezi la kupiga kura lilianza na tayari mshiriki mmoja ambaye ni Rosa Ree ametolewa.

 

“Joto la shindano hili lipo juu sana. Baada ya orodha kamili ya washiriki 20 kuwekwa wazi, zoezi la kupiga kura limeanza kwa kasi ya ajabu na tayari Rosa Ree ametolewa.

 

“Washiriki waliobaki ni Nandy (1), Lulu Diva (2), Lulu (Elizabeth Michael) (3), Kidoa (4), Sanchi (5), Official Lyyn (6), Tunda (7), DJ Sinyorita (8), Amber Lulu (9) na Wolper (10).

 

“Wengine ni V-Money (11), Diana Kimari (12), Poshy Queen (13), Mimi Mars (14), Kim Nana (15), Official Nai (16), Malkia Karen (18), Queen Elizabeth (19) na Sylivia Sebastian (20).

 

“Unachotakiwa kufanya ni kupiga kura ya nani atoke kwa kuandika jina au namba yake ya ushiriki kisha unatuma kwenda WhatsApp namba; 0713 750 910,” alisema Sifael, huku akiwakaribisha wadhamini mbalimbali wa kinyang’anyiro hicho.

Leave A Reply