Ikulu ya Marekani Yapanga Kupunguza Nikotini kwenye Sigara

Ikulu ya Marekani inapanga kupunguza kemikali ya nikotini kwenye sigara

IKULU ya Marekani White House imetangaza mipango ya kupunguza kiwango cha malighafi ya Nikotini kwenye sigara hatua inayosemekana kuwa inaweza kupunguza kiwango cha uwezekano wa kupata maradhi ya saratani (Cancer).

 

Ingawa inasadikiwa kuwa mpango huo unatarajiwa kukumbwa na upinzani mkubwa kutoka kwenye viwanda vya uzalishaji wa tumbaku.

 

Uvutaji umebaki kuwa chanzo kikuu cha vifo nchini Marekani ambapo inakadiriwa zaidi ya watu 480,000 wanafariki kila mwaka, hii ni kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Kupambana na Kuzuia Magonjwa CDC.

 

Kemikali ya Nikotini ina uwezo mkubwa wa kusababisha uraibu kwa mtumiaji kiasi kwamba ikipunguzwa au kuondolewa kabisa inaweza kuwa na madhara chanya kwa watumiaji.

 

Uvutaji wa sigara unasababisha vifo vya zaidi ya watu 480,000 nchini Marekani

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Serikali ya Marekani imesema kuwa:

“Kutengeneza sigara au bidhaa nyingine za tumbaku ambazo zitapunguzwa kemikali ya nikotini inayosababisha uraibu litakuwa ni jambo jema zaidi kwenye kusaidia kunusuru maisha ya watu.”alisema Kamishina wa Mamlaka hiyo Dkt. Robert M Califf.

 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka 2020 zilibainisha kuwa jumla ya watu wazima milioni 30.8 walikuwa wanavuta sigara.2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment