Ikulu ya Nigeria Yakanusha Kifo cha Rais Muhammadu Buhari

SERIKALI ya Nigeria imewataka wananchi wa Nigeria kupuuza uvumi kwamba Rais Muhammadu Buhari hali yake ni mahututi na kwamba huenda amefariki.

Mshauri Mwandamizi wa Rais Buhari kuhusiana na Vyombo vya Habari, Garba Shehu,  amesema uvumi huo “ni uwongo wa wazi unaolenga kuwatia hofu wananchi.”

Baadhi ya uvumi huo ni kwamba rais huyo hivi sasa amewekewa mashine za kumsaidia kupumua na kuna uvumi unaosema kwamba tayari amefariki dunia.

Shehu amewahakikishia wananchi wenzake kwamba wasiwe na wasiwasi wowote na kwamba hakuna chochote kilichomtokea kiongozi wao.

“Kama mmezipata habari hizi kutoka katika mtandao wa WhatsApp au  Facebook, ziuuzeni kwani zina lengo la kuleta hofu.”

Kumekuwapo na habari zilizozagaa duniani kupitia mitandao na vyombo vya habari zikisema rais huyo amefariki dunia, baada ya kuondoka nchini mwake Jumapili iliyopita kwenda kupata matibabu.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment