Mwakilishi wa shilika la kazi duniani nchini (ILO), Getrude Sima amepokea tuzo waliyotunukiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro. ILO ilitunukiwa tuzo hiyo kwa kuwa taasisi iliyomstari wa mbele katika kubadilishana taarifa za masuala ya usalama na afya nchini, kikanda na kimataifa.