Imani Kajula Amkaribisha Bosi mpya wa Simba Uwayezu Francois
Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula akiongea na Afisa Mtendaji Mkuu mteule, Uwayezu Francois Regis baada ya kumkaribisha.
Pamoja na kumpitisha kwenye masuala kadhaa kuhusu klabu Kajula amempa maelezo ya kina juu ya mikakati mbalimbali endelevu ya klabu hiyo ya Msimbazi.
Kama ambavyo umma ulijulishwa hapo awali, Kajula ataendelea kumpatia Regis uwelewa wa mifumo, utendaji kazi, wadau, mikakati na masuala mengine ya klabu hadi Agosti 31, 2024, ambapo Kajula ataondoka rasmi na Regis kushika hatamu ya kazi za Afisa Mtendaji Mkuu.