The House of Favourite Newspapers

INASIKITISHA!! Bibi Abomolewa Nyumba Kwa Nguvu- Video

Bibi Mkazi wa Kijiji cha Mahindu wilayani Misungwi amejikuta akitolewa kwa nguvu katika nyumba yake ili kupisha upanuzi wa barabara baada ya kugoma kubomoa nyumba hiyo kwa mujibu wa sheria.

 

Bibi huyo ambaye awali alikuwa amegoma kutoka kwenye nyumba hiyo akidai malipo huku akilalamika kunyanyaswa kwa kuwa hana mume, (mjane) baadaye alitolewa kwa amri ya mwenyekiti wa wilaya na mwenyekiti wa serikali ya kijiji na wa  kata wakishirikiana na wanakijiji wa eneo jhilo.

 

Akizungumza mara baada ya kubomoa nyumba hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi alisema jambo la kubomoa kibanda kama kile siyo lazima mpaka lifanywe na Rais Magufuli, bali wao kama viongozi wa wilaya na wananchi kwa ujumla wanapaswa kumuunga mkono Rais kwa kutekeleza adhima ya kuboresha miundombinu.

 

Aidha, aliongeza kuwa bibi huyo ameshatengewa eneo jingine la kuishi na kuweka fremu za maduka ili apishe kwenye eneo la barabara hiyo ambayo imeshaingizwa kwenye mtandao wa barabara za halmashauri na mkandarasi ameshaanza kazi rasmi ya ujenzi.

MSIKIE BIBI AKIELEZA MASIKITIKO YAKE

Comments are closed.