The House of Favourite Newspapers

INASIKITISHA! HAMISI ANAVYOTESEKA, UTAMWAGA MACHOZI

WAKATI mimi na wewe tukiwa wazima wa afya, Watanzania wenzetu wanaotekeska kwa maradhi ama shida mbalimbali, si kwa kutaka wao bali kwa mapenzi ya Mungu.

 

Mtazame kijana Hamisi kwenye picha hii akiwa na nafuu na hapa akiwa na hali aliyo nayo kwa sasa! Mtoto huyu alivimba mguu, akapelekwa India kwa matibabu, kutokana michango yenu Watanzania aliongozana na mmoja wa wafanyakazi wa Global Publishers, Imelda Mtema.  Alifanyiwa upasuaji na hali yake ikawa nafuu, akarejea nchini lakini hali yake sasa ni kama unavyomuona.

Inasikitisha sana na kunifanya nitamani nigekuwa na uwezo wa kumwondolea maumivu aliyonayo, lakini hiyo ni kazi ya Mungu Mwenyezi. Hamisi anaishi na ndugu yake katika chumba cha kupanga katika umasikini mkubwa baada ya baba yake kufariki waliporejea kutoka India.

 

Nakuomba kwa mikono yangu yote miwili, uitii sauti ya Mungu inayonena ndani yako hivi sasa na umsadie Hamisi chochote kile ili kufanya maisha yake yawe nafuu kidogo.

 

Najua una shida nyingi lakini namuaomba Mungu uguse moyo wako. Hata shilingi mia mbili uliyo nayo inaweza kubadili maisha yake. Unaweza kumtumia chochote au kumjulia hali HAMISI kupitia namba hii, 0716963026 (italeta jina la FATUMA LWIGILA ambaye ni dada yake). Mungu akubariki sana!

Comments are closed.