NDOTO ya timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji iliota mabawa jana Jumapili baada kufungwa na wenyeji Kenya kwa njia ya penalti na kujikuta wakiangua kilio cha huzuni uwanjani hapo baada ya kushinwa kutwaa ubingwa huo.
Licha ya kupambana kuanzia mwanzo wa michuano hiyo huku wakionyesha ari na molali pamoja na uwezo mzuri, Zanzibar Heroes wanaonolewa na Kocha Hemed Morocco walimaliza dakika 90 wakiwa wamfungana mabao 2-2 na Kenya kwenye fainali hiyo iliyopigwa Uwanja wa Kenyatta nchini Humo.
Zanzibar Heroes waliwastaajabisha wengi baada ya kutoka nyuma mara mbili wakati walipogungwa na kupata sare hiyo lakini wakaja kufungwa kwa penalti 3-2.
Mabao yote ya Zanizbar Heroes yalifungwa na Khamis Mussa huku yale ya wenyeji Kenya yakifungwa na Ochieng Ovellana pamoja na Choka Masoud .
Wachezaji waliokosa penalti kwa upande wa Zanzibar ni Adeyum Seleman, Khamis Mussa na Mohammed Issa “Banka”
Katika Hatua Nyingine timu ya taifa ya Uganda , The cranes waliiibuka washindi wa tatu baada ya kuwafunga Burundi kwa mabao 2-1.


Comments are closed.