The House of Favourite Newspapers

Infantino Awalipua Wazungu, Awataka Waombe Msamaha kwa Waafrika kwa Miaka 300

0
Rais wa FIFA Gian Infantino

RAIS wa FIFA Gian Infantino ameibuka leo na kutoa kauli yenye utata ikiwa imebaki siku moja kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Qatar.

 

Infantino ambaye ni raia wa Switzerland mwenye asili ya Italia amesema kuwa kwa mambo ambayo wazungu wamewafanyia waafrika kwa miaka 300 iliyopita hawatakiwi kuwafundisha chochote na badala yake wanatakiwa kuwaomba msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.

 

Katika hotuba yake ambayo imekosolewa vibaya na vyombo vya Habari vya mataifa ya Ulaya Infantino amesema akiwa Qatar ameonesha kuguswa na wakimbizi, watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja lakini pia anajiona mwafrika wakati huohuo anajiona mwarabu.

Infantino amesema raia wa Ulaya wanatakiwa kuwaomba msamaha waafrika na dunia kwa ujumla kwa miaka 300 ijayo

Infantiono ameyasema hayo ikiwa ni katika jitihada zake za kutetea ufanyikaji wa Kombe la Dunia nchini Qatar jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikosolewa na wadau mbalimbali wa soka hasa wanaotoka mataifa ya Ulaya ambao wanaamini kuwa ilikuwa ni makosa kupeleka mashindano hayo nchini humo.

 

“Najua ni kivipi inamaanisha kunyanyasika na kutengwa, Mimi ni raia wa Ulaya na sit u kwamba najivunia kuwa raia wa Ulaya lakini hakika mimi ni raia wa Ulaya, Nadhani kwa kipindi cha miaka 300 mambo tuliyofanya Afrika na duniani kote kwa ujumla tunatakiwa tuombe msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.” amesema Infantino.

Leave A Reply