visa

INFINIX WALICHOWAFANYIA WATEJA WAO VALENTINE

Afisa Uhusiano wa Infinix Tanzania, Aisha Karupa akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix Mobile Tanzania katika kusherehekea siku ya wapendanao leo imezindua duka jipya maarufu kama Infinix Smart Hub, lililopo Jengo la China Plaza Kariakoo  Dar. Akizungumza na wanahabari Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Aisha Karupa amesema lengo la kufungua duka hilo ni kuzidi kuwafikia wa wateja wake kiurahisi zaidi.

Meneja Masoko wa Ifinifix, Saiphone Asajile akizungumzia simu hizo.

Aisha aliwashukuru Watanzania kwa kuzipokea bidhaa za Infinix na kuwa wateja wao wazuri.  biAisha ameendelea kusema Infinix itaendelea wigo ili kuhakikisha wateja wao wanapata huduma stahiki kama vile simu na bidhaa nyingine za Infinix zenye ubora zaidi zikiwa na waranti ya mwaka na mwezi mmoja pamoja na kutoa elimu bure kuhusiana na utunzaji na utumiaji wa simu za Infinix kwa muda mrefu bila kuwasumbua wala kuwaletea shida yeyote.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Saiphone Asajile naye alieleza machache kuhusiana na mauzo ya simu ya kisasa kabisa aina ya Infinix, tangu ilipoingia hapa nchini mwaka 2018 na kuonesha ubora wa hali ya juu kwa watumiaji wake.

Matukio katika picha:

Wahudumu wa Infinix wakiwahudumia wateja waliofika kwenye duka hilo.

Wahudumu katika lango la kuingilia duka hilo jipya.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL 
Toa comment