The House of Favourite Newspapers

Injinia Afunguka Kutembea Na Risasi Mwilini “Aliyenipiga Amepigwa Faini Ya Mil. 2 Tu” – Video

0

Februari 18, 2023, ni siku iliyobadilisha kabisa maisha ya kijana Gerdat Mfyoa. Yeye na ndugu zake, walikuwa wametoka ‘out’, wakati wanarudi nyumbani kwa kutumia gari lao, kijana mmoja mwenye asili ya Kiarabu, aliwagonga kwa kutumia gari yake kwa makusudi na hakutaka kusimama.

Walipomfuatilia mpaka anapoishi, ndipo sekeseke kubwa lilipoibuka na kusababisha Gerdat apigwe risasi ambayo imeshindikana kutolewa mwilini mpaka leo.

Ndugu zake nao walishambuliwa vibaya na kijana huyo wa Kiarabu na wenzake takribani nane!

Kesi ikapelekwa mahakamani, miezi takribani nane baadaye, hukumu ikatoka ambapo kijana huyo alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kulipa faini ya shilingi milioni 2.6, jambo lililofanya Gerdat na familia yake wapinge hukumu hiyo na kukata rufaa.

Siku zinazidi kuyoyoma, rufaa bado haijasikilizwa, Gerdat bado anatembea na risasi mwilini, aliyempiga anadunda mitaani!

Leave A Reply