#GlobalUpdates: Instagram Kuruhusu Posts Za Picha, Videos Mpaka 10 Kwa Wakati Mmoja!
Kwa wale watu wangu ambao hupata wakati mgumu kuchagua picha ama video gani ya kupost Instagram, usijali Instagram wana solution kwa ajili yako: Zipost zote, kwa wakati mmoja!
Leo nimetembelea mtandao wa Instagram na kuona kuwa wameisogeza kwetu update mpya itakayokuruhusu wewe mdau kupost picha na video 10 kwa wakati mmoja kwenye post moja.
Followers wako wakitembelea page yako na kuona post hiyo wataweza pia kuona na picha nyingine zote ndani ya post hiyo bila wewe kupost picha nyingi ya tukio moja ama matukio tofauti, yote unaweza kuyakusanya na kuyaweka kwa pamoja bila stress.
Kwa mujibu wa Instagram, mabadiliko haya ya namna ya kupost na kushare picha na videos yametokana na utafiti walioufanya na kugundua kuwa watu wengi mara nyingi hushindwa kufanya maamuzi ya picha gani ama video gani na ya kushare na followers wao…
“With this update, you no longer have to choose the single best photo or video from an experience you want to remember. Now, you can combine up to 10 photos and videos in one post and swipe through to see them all.” – Instagram.
So, Unapost vipi?
- Ukiwa unataka ku-upload kitu kutoka kwenye gallary yako, utaona ki-icon kipya kitakachokuruhusu kuchangua picha na videos zaidi ya moja. Hii inasiaida kupanga jinsi ambayo utataka post yako ionekane kwa followers wako.
- Unaweza pia kubadilisha order ya mpangilio wa picha au video zako kwa kupress & hold picha au video husika.
- Kisha weka filter moja kwa picha ama video zote au edit picha moja moja au video moja moja kwa filter uzipendazo.
- Andika caption yako kisha post kwenye timeline yako.
Kwenye ‘Instagram feed’ yako utaona vidoti vya blue kwa chini ya hizi posts, vidoti hivi vinakuruhusu kuswipe na kuona picha au video nyingine zote na unaweza ukalike video ama picha moja kati ya zile 10 zilizopostiwa na ku-comment pia kama kwenye post ya kawaida.
Kwa sasa post hizi zinakuruhusu kuweka caption moja tu mpaka pale Instagram watakapotusogezea uwepesi mwingine.
Hapo awali udate hii ilikuwa inapatikana kwa watu wenye page za kibiashara lakini kuanzia leo update hii inapatikana dunia nzima kwa watumiaji wote wa Instagram.
Update your Instagram and enjoy!
IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.
Comments are closed.