The House of Favourite Newspapers
gunners X

IRAN: Wafungwa waachiwa huru kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona

0

Iran imewaachia huru kwa muda wafungwa zaidi ya 54,000 ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona katika magereza yaliyo na msongamano wa watu. Msemaji wa mahakama Gholamhossein Esmaili amewaambia waandishi wa habari kuwa wafungwa waliruhusiwa kutoka gerezani baada ya kupimwa na kukutwa hawana ugonjwa wa Covid-19(virusi vya corona). Wafungwa wa usalama waliofungwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitano hawataachiwa.

Mfanyakazi wa wahitaji nchini Iran ambaye ni raia wa Uingereza, Nazanin Zaghari-Ratcliffe anaweza kutolewa hivi karibuni kwa mujibu wa mbunge wa Uingereza . Balozi wa Uingereza nchini Iran,Tulip Siddiq alisema kuwa bi Zaghari-Ratcliffe ataachiwa huru leo au kesho.

 Zaghari-Ratcliffe

Mume wake alisema siku ya jumamosi kuwa aliamini mke wake alipata maambukizi ya Covid-19 akiwa gereza la Evin laTehran na mamlaka yalikuwa yanakataa kumpima. Lakini bwana Esmaili alisisitiza siku ya jumatatu kuwa Zaghari-Ratcliffe alikuwa akiwasiliana na familia yake na kuwaambia kuwa afya yake iko salama.

Bi.Zaghari-Ratcliffe alifungwa kwa kipindi cha miaka mitano mwaka 2016 baada ya kukamatwa alikanusha kuhusika na madai yanayomkabili.Huku Uingereza ikisisitiza kuwa bi Zaghari hana hatia. Msemaji wa ofisi ya mambo ya nje alisema kuwa serikali ya Iran itawaruhusu haraka wataalamu wa afya kuingia katika gereza la Evin kuangalia hali za raia wenye uraia wa Uingereza na Iran zikoje.

Mpaka sasa zaidi ya kesi 90,000 za ugonjwa wa Covid-19 duniani kote zimeripotiwa na vifo3,110 tangu ugonjwa huu uanze mwishoni mwa mwaka jana, huku wengi waliokufa ni wachina . Mlipuko wa virusi vya corona umeuwa watu wapatao 77 nchini Iran kwa muda usiozidi wiki mbili.

Siku ya Jumanne, wizara ya afya imesema kuwa idadi ya visa vya corona vilivyothibitishwa ni zaidi ya asilimia hamsini. Kwa sasa ni watu 2,336, ingawa inaaminika kuwa takwimu i kubwa zaidi ya inayotajwa. Kesi zinazohusisha Iran zimeripotiwa Afghanistan, Canada, Lebanon, Pakistan, Kuwait, Bahrain, Iraq, Oman, Qatar na Nchi za falme za kiarabu.

Kwa sasa wazriri wa afya Saeed Namaki alisema kuwa wanaanzisha kampeni ya upimaji wa virusi hivyo ambayo itaanza siku ya Jumatano. Wahudumu wa afya watawatembelea wagonjwa ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya Covid-19 na hawana huduma ya afya.

Kundi ya wataalamu wa afya kutoka shirika la afya duniani(WHO) iliwasili Iran siku ya Jumatatu ili kuisaidia mamlaka ya Iran. WHO imesema kuwa ikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 15,000 na vifaa vya maabara zaidi ya 100,000.

Chanzo :Bbcswahili

Leave A Reply