The House of Favourite Newspapers

IRAN YAMPUUZA TRUMP NA VITISHO VYAKE

Waziri wa mambo  ya kigeni nchini Iran Javad Zarrif amepuuzia vitisho vya  Rais wa Marekani Donald Trump juu ya kuliangamiza taifa la Iran iwapo litajaribu kupigana na Marekani.

Waziri Zarif amesema kuwa rais huyo wa Marekani anafaa kutazama historia ya nyuma, ambayo inaonesha namna Iran ilivyoshinda vita vyote dhidi ya wachokozi wake.

Rais Trump alituma ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili akisema: Iwapo Iran inataka kupigana na Marekani hiyo ndio utakuwa mwisho wa taifa hilo.

Na wakati huo huo Msemaji wa shirika la kawi ya Atomiki Behrouz Kamalvandi, amesema kuwa Iran itazidisha kiwango cha uzalishaji wa madini ya Uranium na kuzidisha kiwango ilichowekewa katika siku za usoni.

Comments are closed.