The House of Favourite Newspapers

IRENE MWAMFUPE KUANDIKA HISTORIA J’PILI

Irene MwamfupeM WANAMUZIKI wa Nyimbo za Injili, Irene Mwamfupe, anatarajia kuandika historia kubwa Jumapili hii katika uzinduzi wa albamu yake ya Hodari.

 

Irene alisema uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika ndani ya Kanisa la Mito ya Baraka, Kariakoo jijini Dar, utakuwa wa kipekee kutokana na orodha kubwa ya wanamuziki ambao wamejitoa kutumbuiza akiwemo Bahati Bukuku, Happy Mlinga, Mariam Kilyenyi, Martha Mwaipaja, na Edda Mwampanga.

 

Irene alisema siku hiyo itakuwa ni siku njema ya kumsifu Mungu na itakuwa ni siku ya kupokea miujiza kupitia sifa. “Mungu wetu hukaa katikati ya sifa kwa hiyo Jumapili hiyo atakaa katikati yetu na tutapokea mahitaji yetu kwa sababu tumeacha vyote na kujumuika pamoja kumsifu Yeye Bwana.

 

“Niwakaribishe watu wote, hakutakuwa na kiingilio, waje washuhudie uzinduzi wa albamu yangu ya Hodari na pia wataweza kuwasikia na kuwaona wanamuziki wenzangu wa muziki wa Injili,” alisema Irene.

 

Irene alisema mbali na waimbaji hao, waimbaji wengine watakaoupamba uzinduzi wake ni pamoja na Mchungaji Bonny Mwaitege, Mchungaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Emmanuel Mbasha, Madam Ruth, Happy Mlinga, Edda Mwampagama na kwaya zote za Mito ya Baraka ambazo ni Jerusalem Choir, Rhema Kwaya, Ebenezer Kwaya, WWI Kwaya na The Joshua Generatio.

Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.