Irene Paul Adaiwa Kupotezwa Na Ndoa

Bongo Muvi, Irene Paul.

MSANII kiwango kunako soko la Bongo Muvi, Irene Paul anadaiwa kupotezwa na ndoa na kwamba kwa sasa haonekani kwenye tasnia hiyo.

 

Kwa mujibu wa chanzo, Irene anayesifika kuzitendea haki ‘scene’ zake anazopewa hususan kwenye suala zima la ‘ung’eng’e’, tangu ameolewa amekuwa hasikiki tena kwenye filamu kama ilivyokuwa awali.

 

“Hii ni ndoa tu itakuwa imempoteza, zamani alikuwa tishio kwenye kila filamu anayotoa iwe ameshirikishwa au amecheza mwenyewe lakini tangu ameolewa amekuwa kimyaa,” kilibonyeza chanzo hicho.

 

Star Mix lilimtafuta, Irene kujibu madai hayo ambapo alifunguka:

“Ndoa si kwamba inamfanya mtu awe kimya, nipo kimya kwa sababu nina biashara zangu nyingine.”

STORI NA IMELDA MTEMA | IJUMAA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment