IRENE PAUL: Situmii Gharama Kujichubua!

Irene Paul

MWIGIZAJI mkali anapokuwa mbele ya kamera, Irene Paul ameamua kuwahamasisha mastaa na watu mbalimbali kuepuka gharama ya kujitengeneza badala yake wanaweza kubaki na uasili wao na wakapendeza.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Irene alisema amekaa na kujitathimini na kugundua kuwa hatumii gharama kubwa kununua nywele za bei mbaya au kutumia madawa ya usoni, lakini bado anaonekana mrembo.

 

“Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu,” alisema Irene

Loading...

Toa comment