The House of Favourite Newspapers

IRENE PAUL: Bado Nitaendelea Kuzaa

MREMBO Bongo Movies, Irene Paul amefunguka kuwa sio kwamba ameweka nukta kwa kuzaa mtoto mmoja bali anamuomba Mungu, azidi kumpa nguvu kwani anatarajia kuongeza mtoto mwingine wa pili kwani hana hofu na kuzeeka mwili wake au kupoteza muonekano alionao.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Irene alisema kuwa kwa hivi sasa mambo mengi yamebadilika sana furaha ya watu wengi ni watoto hivyo yeye anaona wazi akizaa haraka ataweza kuitengeneza akili yake kupanuka zaidi na kumpa nguvu ya kufanya vitu vingi kwa ajili ya familia yake ya baadae.

“Sina hofu na kuendelea kuzaa labda kuhofia nitapoteza muonekano wangu au nitapoteza ustaa wangu ninachojua ni kwamba watoto wanafanya akili kuchangamka na kila mtu anajivunia kuwa na watoto wake tofauti na huko nyuma wengine walikuwa wanawaficha,” alisema Irene Paul.

Comments are closed.