ISABELA, BABY MADAHA NDANI YA BIFU ZITO

Isabela Mpanda

WASANII wa muziki wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda na Baby Madaha wanadaiwa kuwa ndani ya bifu zito.  

 

Chanzo cha habari kiliiambia Mikito Nusunusu kuwa wawili hao ambao walikuwa marafiki walioshibana kwa sasa wamekuwa maadui chanzo kikitajwa ni Baby Madaha kutohudhuria mazishi ya dada wa Isabela ambaye alifariki dunia hivi karibuni.

Alipoulizwa Isabela kuhusiana na hilo alisema ni kweli hampendi Baby Madaha na urafiki wao umeshavunjika kwani alishindwa kumpa ushirikiano alipofiwa na dada yake jambo ambalo linamuumiza mpaka sasa.

“Kitendo cha kutokuja kwenye msiba wa dada yangu kiliniuma sana na mpaka sasa naumia maana Baby Madaha ni rafiki yangu wa damu, aliniachia msiba nizike peke yangu na anajua fika kwamba yeye ndiye rafiki yangu mkubwa nimekasirika sana huo ndiyo ukweli,” alisema Isabela. Kwa upande wa Baby Madaha alisema hana bifu na Isabela na mwenyewe anajua kwa nini hakuhudhuria kwenye msiba wa dada yake kwani alikuwa nje ya nchi ndiyo maana

Stori: Neema Adrian

Loading...

Toa comment