The House of Favourite Newspapers

Isabella atumika kuwauza wasichana mtandaoni

0

ISABELA.pngNa Hamida Hassan

‘MUUZA nyago’ kupitia muziki na filamu hapa Bongo, Isabella Mpanda amekwaa skendo ya kuuza wasichana kwa mapedeshee, kufuatia jina lake kutumiwa na mtu ambaye jina lake halisi halikupatikana mara moja, ambaye anajitambulisha kwa jina la msanii huyo.

Mpashaji wa habari hii ambaye ni rafiki wa karibu na Isabella aliliambia gazeti hili kuwa, mhalifu huyo wa mtandaoni, anatumia picha ya Isabella kuwataka wanaume wenye pesa wamuone na yuko tayari kuwaunganisha kwa wasichana wazuri wa mjini.

Isabella alipoulizwa juu ya habari hiyo alikiri kukumbana na kadhia hiyo, ambapo alisema: “Nimempata huyo mtu, anaitwa Angel, nilimpigia simu akaniomba msamaha akidai kuwa njaa imemsukuma kufanya hivyo, nimemsamehe lakini kwa onyo kali la kutorudia upuuzi wake huo.”

Leave A Reply