Isha Mashauzi: Corona Ikipita Tu, Kazi Kama Dawa

KUTOKANA na mikusanyiko mbalimbali ikiwemo shughuli za muziki kusitishwa kutokana na Virusi vya Corona, prezidaa wa Kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ amesema anaamini janga hilo likipita muziki utarudi kuwa juu kama ulivyokuwa enzi zake.

 

Isha aliiambia Amani kuwa baada ya kipindi hiki kupita, wadau wengi wa burudani watakuwa na kiu ya burudani ambayo watakuwa wameimisi kwa muda mrefu, hivyo itasababisha muziki kurudi sehemu yake kama ulivyokuwa mwanzo.

 

“Kwa kipindi hiki niwashauri wanamuziki wenzangu kutumia muda huu kuwaza kazi za maana ili tukishafunguliwa tusikose jipya la kuwapa mashabiki zetu.

 

“Kipindi ambacho mashabiki wengi watakuwa na kiu ya burudani, ndiyo nafasi ya kurudi kwa muziki ambao ulikuwa umeshapoteza mashabiki,” alisema Isha.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment