The House of Favourite Newspapers

Ishara 4 Rayvanny Kurudiana na Fahyma

0

KUNA msemo usemwao mapenzi ya kweli hayafi na hata yakifa hayaozi na hata kama ikitokea yakaoza, basi hutoa harufu ya marashi mazuri zaidi.

 

Msemo huo unathibitishwa na lililokuwa penzi zito kati ya mrembo mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Faima Msenga ‘Fahyma’ na staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambao miaka kadhaa nyuma walipendana mno hadi wakafikia hatua ya kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jayden.

 

Lakini kwa bahati mbaya, baadaye walitengana huku sababu kubwa ikidaiwa ni usaliti na mwanamke kupenda maisha ya gharama kuliko uwezo alionao, hali iliyomfanya Rayvanny ahamishie majeshi kwa mrembo Paula Kajala; binti mdogo na mbichi.

 

Baada ya siku kadhaa tangu Paula atimkie nchini Uturuki kwa ajili ya masomo yake ya ngazi ya juu (chuo) huku nyuma vibweka vikaanza upya ambapo kuna ishara nne (4) zinazosababisha watu waamini kuwa huwenda Rayvanny na Fahyma wamerudiana.

 

KOTI

Siku moja tu tangu Paula aondoke nchini, Fahyma aliposti video kwenye Insta Story yake akiwa njiani kuelekea mkoani Kilimanjaro akiwa amevaa koti lenye rangi nyeusi ambalo inadaiwa ni la Rayvanny, hivyo walimwengu wakaunganisha doti kuwa huwenda mahaba yakawa yamesharudi upya.

 

VITANDA KUFANANA

Baada ya mrembo huyo kuwasili kutoka mkoani Kilimanjaro alikokuwa amekwenda kwa ajili ya kutangaza bidhaa f’lani, alijirekodi tena video akiwa amelala kwenye kitanda ambacho siku chache alionekana Rayvanny akiwa amekilalia.

 

Lakini baada ya Fahyma kuulizwa imekuwaje alalie kitanda kinachofanana na cha Rayvanny, alijibu kwa ufupi tu kuwa, siyo kweli kwamba alilala kwenye kitanda alicholalia Rayvanny na pia vina utoafauti kwa sababu kitanda chake ni cha rangi ya maziwa na cha Rayvanny ni cheupe.

 

“Kama mmeangalia vizuri kile kitanda mtagundua kina tofauti, kitanda changu kina rangi ya maziwa, lakini cha Rayvanny ni cheupe kabisa,” alisema Fahyma

 

FAHYMA NA NYIMBO ZA RAYVANNY

Jambo lingine lilofanya baadhi ya watu wahisi kuwa huwenda wawili hao wakawa wamerudiana kwa siri ni baada ya hivi karibuni Fahyma kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anaburudika na Wimbo wa Rayvanny wa Baila na kuacha watu midomo wazi.

 

WADAIWA KUONEKANA PAMOJA

Hii ndiyo kubwa kuliko kwani mapema wiki hii, wawili hao walidaiwa kuonekana pamoja katika mgahawa mkubwa ambao Rayvanny anadaiwa kuutangaza uliopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar huku wakipeana mahaba kama yote.

 

Baadhi ya watu wameonekana kufurahia jambo hilo na wengine wameonesha kutopenda hadi kufikia hatua ya kumsema vibaya Fahyma kuwa akiachwa aachike kuliko kujipendekeza kila siku kwa mwanaume ambaye kwa sasa ameamua kumficha na hataki kumuweka hadharani tena na kumpa heshima yake kama mzazi mwenzake.

STORI; WAANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply