ISHI KITUZO NA VODACOM ‘TUZO POINTS’ UJIPATIE VIFURUSHI
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom katika kuboresha huduma za mawasiliano kwa Watanzania, imezindua huduma mpya iitwayo Tuzo Points ambapo watumiaji wa mtandao huo, sasa watakuwa na uwezo wa kujikusanyia pointi kadiri wanavyozidi kutumia huduma mbalimbali za mtandao huo.
Pointi hizo, zimegawanywa katika makundi mbalimbali ambapo mteja wa huduma ya malipo ya kabla, atakuwa akipata zaidi kulingana na huduma anayotumia, kuanzia kuongeza salio mpaka kwenye makato yatokanayo na miamala ya M-Pesa kisha kuzitumia pointi hizo kufanya manunuzi mbalimbali yakiwemo ya vifurushi, simu na mengineyo.
MTEJA ANAPATAJE TUZO POINTI?
Ili kunufaika na huduma hii mpya, mteja wa Vodacom anatakiwa kuendelea kuongeza salio na kufanya miamala mbalimbali katika simu yake. Katika kila shilingi 10 ya salio la muda wa maongezi atakayoongeza mteja, atapata pointi 1. Ufuatao ni mchanganuo wa jinsi mteja anavyoweza kujishindia pointi:
JINSI YA KUTUMIA POINTI
Baada ya kujikusanyia pointi za kutosha, mteja wa Vodacom anaweza kuzitumia kununua vifurushi au hata kuzibadilisha pointi hizo kuwa fedha kupitia M-Pesa. Mteja anaweza kutumia pointi hizo kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Pointi kwa wakala yeyote wa M-Pesa.
Namna ya kutumia pointi hizo, mteja ataingia katika menu ya simu yake na kupiga namba *149*01#> TUZO> TUZO POINTI> VUNA POINTI> (Nunua Kifurushi/ Lipa kwa Pointi/ Hamishia kwenye M-Pesa).
Pia mteja anaweza kuangalia salio la pointi zake kwa kupiga *149*01# kisha chagua “TUZO” kisha TUZO POINTS.
Vifuatavyo ni vifurushi ambavyo mteja anaweza kununua kwa kutumia Tuzo Pointi:
TUZO pointi ambazo mteja atazipata zitadumu kwa muda wa miezi 12 tangu siku ya kuzipata. Kama pointi hazijatumika ndani ya kipindi hicho, zitaondolewa kwenye akaunti ya mteja. Pia kama mteja hajatumia mtandao wa Vodacom kwa muda wa siku 60, atapoteza pointi zote alizozikusanya.
Comments are closed.