Ishu Mpya Yaibuka Makipa Yanga

KIPA wa Yanga, Metacha Mnata amekiri kuwa hali ni tete kwenye ushindani baina yao kwani mpaka sasa hana uhakika wa kuwa kipa namba moja licha ya kudaka mechi zote za kimataifa.

 

Metacha anasema kwamba mapambano ya dhidi yake na makipa wenzie Mkenya, Farouk Shikalo na Ramadhani Kabwili kuwania namba ni makubwa na anaona lolote linaweza kutokea muda wowote kwavile kila mmoja ana uwezo na anaonyesha juhudi kubwa mazoezini.

 

Metacha alisajiliwa na Yanga msimu akitokea Mbao FC na tayari amedaka mechi tatu za mashindano ambazo ni za Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Township (2) na Zesco United pale Taifa. Kabla ya mechi ya jana, kipa huyo kwenye mechi hizo hakuna mchezo ambao amefungwa mabao mawili ingawa ingawa ameruhusu mabao matatu kwenye mechi tatu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, kipa huyo alisema; “Unajua kila mchezaji anapambana na lengo ni kuwa bora na kuonekana na timu zile kubwa ndiyo maana unakuta mimi naweka bidii kwa kufanya vizuri kila ninapopata nafasi.”

 

“Nataka kuwa bora na kuwa wa kimataifa ndiyo maana napambana kufikia malengo yangu japo
ushindani ni mkubwa kama hapa tupo makipa wote wazuri na wenye uwezo lakini utapangwa kutokana na uwezo wako,”alisema Metacha.

 

Kipa huyo aliwahi kuibuka kuwa kipa bora wa michuano ya Sportpesa Super Cup ambayo ilifanyika hapa nchini mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Loading...

Toa comment