Ishu ya Ajibu Kufeli TP Mazembe Yavuja

BAADA ya dili la Ibrahim Ajibu Migomba kutoka Yanga kwenda TP Mazembe ya DR Congo kufeli, mapya yamevuja. Kumbe mshikaji alitaka Mil 20 kwa mwezi.

 

Mmoja wa makomandoo maarufu wa TP Mazembe, Patrick Mazembe, ameliambia Spoti Xtra kuwa; “Unajua wachezaji wakisikia wanatakiwa na TP Mazembe huwa wanahitaji vitu vingi kwa kuwa wanajua kuwa tuna fedha, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mchezaji Ibrahim Ajibu na ndio maana tulishindwana.”

 

Kitenge ambaye anaaminiwa sana na uongozi na anasafi ri na timu popote aliongeza kuwa; “Ajibu alihitaji mshahara wa Sh milioni 20 kwa mwezi, nyumba ya kuishi na familia yake pamoja na gari kwa ajili ya kutembelea.

 

“Vitu hivyo ndivyo vilichangia dili hilo kukwama kwani Mazembe walikuwa wapo tayari kumpa kila kitu ikiwemo nyumba na gari ya kutembelea, lakini aliambiwa apunguze mshahara, akagoma, hivyo tukashindwana,” alisema.

 

Lakini habari kutoka Yanga zinadai kwamba mchezaji huyo alishasaini dili la awali na Simba ndio maana akawa anawajibu Mazembe anavyotaka.


Loading...

Toa comment