The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Madawa: Wasanii Waitikia wito wa Makonda Kufika Polisi

WASANII wa Bongo wameitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda wa kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam mapema leo asubuhi.

RC Makonda jana aliwataja wasanii 9 wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya pamoja na baadhi ya askari polisi huku akiwataka wafike kwenye Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi kwa ajili ya mahojiano.

Mmoja wa watuhumiwa, Msanii Babuu wa Kitaa akiwasili Kituo Kikuu cha Polisi saa 4: 38 asubuhi
Msanii T.I.D naye akiwasili kituoni hapo saa 5:07 asubuhi huku akishuhudiwa na wanahabari.
Msanii Hamidu Chambuso aka ‘Nyandu Toz’ akiwasili kituoni hapo akiwa ndani ya kazu saa 5: 38.

Wanahabari wakichukua matukio kituoni hapo.

Mwingine ambaye mpaka sasa ameshawasili ni Mmiliki wa Klabu ya Usiku ya Element aliyewasili majira ya saa 5.00 akiambatana na mawakili wake wawili.
Wasanii na polisi waliotajwa na Makonda.

VIDEO: Makonda Awataja Polisi, Wema, TID, Rachel Kuhusika na Mtandao wa Madawa ya Kulevya:

Save

Comments are closed.